moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Ongezeko la uhitaji wa wataalamu wa sekta ya usafiri wa anga , limeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazochukua nafasi muhimu katika kuzalisha na kuandaa wataalamu wa anga barani Afrika.

Chuo cha Usafiri wa Anga [CATC] kilicho chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania [TCAA] kimeendelea kuwa kitovu cha mafunzo ya kisasa.

Mafunzo hayo yanatambulika kimataifa chini ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga [ICAO], kikivutia wanafunzi kutoka zaidi ya nchi 19 barani Afrika na nje ya bara hilo.

Akizungumza na M24 TANZANIA katika mahojiano maalum kwenye maonesho ya SABASABA, Mkuu wa Mafunzo wa CATC, Didacus Mweya, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa.

"CATC ni taasisi inayotoa mafunzo ya viwango vya kimataifa ndani ya nchi, jambo linalosaidia kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika kupeleka wanafunzi nje ya nchi," amesema.

Amesema chuo hicho sasa kinatoa zaidi ya kozi 90 hivi sasa zinazohusiana na sekta ya anga, zikiwemo uongozaji wa ndege, usalama wa anga, teknolojia ya urambazaji.

CATC iliona vema pia kuongeza pia kozi nyingine ya mafunzo ya matumizi ya ndege zisizo na rubani [drone].

Mweya amesema maendeleo ya teknolojia yameongeza mahitaji ya ujuzi mpya katika sekta ya anga, hususan katika maeneo ya kidijitali na mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa huduma za anga.

Hata hivyo, amesisitiza matumizi ya teknolojia hizo lazima yaendane na uelewa wa sheria na taratibu za anga ili kuhakikisha usalama wa ndege za abiria na watumiaji wengine wa anga.

Mweya amesema kupitia chuo hicho Tanzania imeendelea kuzalisha wataalamu wabobezi na wenye uwezo wa kutoa huduma ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo inaiongezea Tanzania ushindani chanya katika sekta ya anga kimataifa.

Mamlaka hiyo imewahimiza vijana kutumia fursa zilizopo kujifunza taaluma za anga, ikisisitiza kuwa sekta hiyo bado ina nafasi kubwa ya ajira na mchango katika maendeleo ya taifa.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement