Mapema alfajiri tayari walikuwa wamefika katika ofisi za Shujaa Cancer Foundation zilizopo huko Mikocheni, Dar es Salaam, tayari kuanza safari kuelekea Kijiji Beach Kigamboni.
Kila mmoja alikuwa mwenye sura ya bakhshasha. Akitarajia mambo mengi ya furaha, kubadilishana mawazo miongoni mwa kila mmoja.
Si unajua 'mtoko' ili unoge lazima muziki uwepo, michezo mbalimbali na msosi bila kusahau vinywaji, hakuna kilichokosekana siku hii.
Juni 7, kila mwaka ni Siku ya Mashujaa wa Saratani Duniani, Mkurugenzi wa SCF Gloria Kida anasema huwa inatumika kukumbushana mambo muhimu pia kuwaenzi waliotangulia mbele za haki.
Zaidi ya kusherehekea, siku hiyo pia huwa ni fursa ya kuimarisha uelewano kati ya walionusurika na wagonjwa wapya, wakipata nafasi ya kubadilishana uzoefu unaojenga matumaini mapya ya kuendelea na maisha.
Pia, ni muda muhimu wa kuondoa hofu na unyanyapaa unaozunguka saratani katika jamii, kwa kuonesha wazi kuwa ugonjwa huo unaweza kutibiwa na maisha kuendelea kwa nguvu mpya baada ya matibabu.
Kwa ujumla, tukio hilo limekuwa zaidi ya burudani ni safari ya matumaini, mshikamano na uthibitisho kwamba baada ya changamoto ya saratani, bado kuna uhai, furaha na ndoto mpya.
Mambo ya 'maakuliiii'Hizi ni baadhi tu ya picha kutoka kwenye tukio hilo, ujumbe mahususi 'kuna maisha baada ya saratani'. unaweza kusoma makala kuhusu yaliyozungumzwa na kujadiliwa kutoka huku, kupitia links hizi...
https://m24tzmedia.blogspot.com/2026/06/saratani-bado-mzigo-maumivu-gharama.html
🔗 Read full article (English)
https://m24tzmedia.blogspot.com/2026/06/cancer-still-heavy-burden-pain-costs.html

Chapisha Maoni