moja

Responsive Advertisement


*Yasema ni mfano bora kuigwa na Klabu zingine *Waandishi wapya zaidi ya 60 wajiunga, 20 wasubiri uhakiki 

Na Mwandishi maalum

Hali ya utulivu, umoja na mshikamano ndani ya Klabu ya Waandishi wa Dar es Salaam (DAR-PC), umeuvutia Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania UTPC) na kupongeza.

Kwa mara ya kwanza, tangu uongozi mpya ulipoingia ofisini kutekeleza majukumu yake ya kazi, ikiwa mwaka mmoja umetimia kufikia sasa, UTPC imefanya ziara katika ofisi za DAR-PC.

UTPC imetambua juhudi kubwa iliyofanywa na uongozi wa DAR-PC chini ya Mwenyekiti Bakari Kimwanga katika kurejesha mazingira rafiki ya kitaaluma.

Hatua ambayo imeanza kuzaa matunda ikiwamo kuongeza hamasa kwa waandishi wa habari wapya hususan vijana kujiunga na klabu hiyo.

Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya amesema sasa wanaona kuna uthabiti wa kiutendaji (stability), unaowezesha wanachama kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa mshikamano.

“Nidhamu ni msingi wa uendeshaji wa klabu, na sisi kama UTPC tunaelekeza nguvu zaidi katika kushughulika na wanachama ili kuhakikisha misingi ya taaluma inalindwa,” amesema.

Mwenyekiti wa DAR-PC Bakari Kimwanga amesema uongozi umeweza kufikia hatua hiyo kwa sababu ya imani kubwa ya wanachama wenyewe pamoja na ushiriki wao.

"Kwa kiwango kikubwa imetusaidia kufungua ukurasa mpya wa maendeleo na kuondoa mtazamo wa kujifungia katika mazoea yasiyokuwa na tija," amesema.

Kimwanga ameongeza "Hatua ya kufanya marekebisho ya katiba kwa ridhaa ya wanachama wenyewe imeongeza nidhamu na uwajibikaji ndani ya klabu. 

"Aidha, utaratibu wa kuwapeleka viongozi kwa awamu kushiriki vikao mbalimbali, umeimarisha umoja na kuongeza hamasa ya wanachama.

"Kutokana na mazingira hayo chanya, klabu hiyo imepokea zaidi ya wanachama wapya 60, na kuna wengine zaidi ya 20 wanasubiri kupitishwa na bodi," amesema.

Amesema DAR-PC ipo makini katika kuhakiki vigezo vya waombaji ikiwamo nakala zao za vyeti vya kitaaluma, ithibati ili kuhakikisha wanaojiunga kweli wanakidhi vigezo.

Kaimu Rais wa UTPC Frank Leonard amesema wataendelea kushirikiana na DAR-PC ikiwa ni pamoja na wanachama wake kupatiwa fursa mbalimbali za kimafunzo.

"Lengo letu ni kuhakikisha taaluma ya uandishi wa habari inaendelea kuimarika chini ya misingi ya maadili, umoja na uwajibikaji," amesisitiza.

Pamoja na hayo, Patricia Kimelemeta ambaye ni mwanachama mwa DAR-PC miongoni mwa vinara wa Program ya Malezi na Makuzi ya Mtoto iliyo chini ya UTPC  ameeleza namna ulivyomjenga.

Ameahidi kuendelea kuelimisha jamii kwa maarifa aliyopata katika mradi huo pamoja na kuwajengea uwezo waandishi wengine wa DAR-PC.

Uongozi wa DAR-PC umesisitiza upo tayari kuendelea kupokea maelekezo na ushirikiano kutoka UTPC.

Umetoa rai kwa wanachama kuendelea “kuchapa kazi” na kulinda maadili ya taaluma ili kuendeleza mafanikio yaliyopo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement