moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Ushindani ni mkali hivi sasa katika sekta ya habari kutokana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na kipindi cha zama za kidigitali.

Suala linaloibua hoja ya uaminifu kwamba ni mtaji mkubwa kwa zama za sasa kuliko hata idadi ya wasomaji na watazamaji.

Ndiyo maana utekelezaji wa mfumo wa ithibati kwa waandishi wa habari na watangazaji unatajwa ni hatua muhimu ya kimkakati ya kuimarisha hadhi ya taaluma hiyo.

Sambamba na hilo ithibati inatajwa ni hatua muhimu ya kusaidia kuimarisha hali yauchumi wa vyombo vya habari nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari [JAB] Wakili Patrick Kipangula amesema hayo mapema hii leo,

alikuwa akiwasilisha mada katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji [ABC 2026] uliofanyika, Jijini Dodoma.

Mfumo wa ithibati umejengwa katika misingi ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Wakili Kipangula amesema una lengo la kuweka viwango vya kitaaluma, kuimarisha maadili na kuhakikisha uwajibikaji ndani ya tasnia.

“Ithibati si chombo cha kudhibiti maudhui ya habari. Ni mfumo wa kulinda hadhi ya taaluma na kujenga imani ya umma kwa vyombo vya habari,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa katika mkutano huo, zaidi ya waandishi 3,200 kati ya 3,900 walioomba vitambulisho vya uandishi wa habari [Press Card] tayari wamethibitishwa.

Ni mara baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kisheria. Idadi hiyo inaashiria mwitikio mkubwa wa wadau katika kujiimarisha kitaaluma.

".., katika soko la sasa la habari, vyombo vinavyowekeza katika weledi wa rasilimali watu wake ndivyo vinavyokuwa na nafasi kubwa ya kuvutia matangazo, wawekezaji na ushirikiano wa kimataifa,".

Amesisitiza hayo Wakili Kipangula katika mkutano huo uliohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya utangazaji.

Wadau hao ni pamoja na Mtandao wa Mabloga Tanzania [TBN] pamoja na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania [JUMIKITA].

Jukwaa la Wahariri Tanzania [TEF], MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania [MCT], MISA Tanzania na EACO.

Mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili mfululizo Februari 12 & 13, 2026 uliandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA].

Mkutano huo ulienda sambamba na maadhimisho ya siku ya redio duniani ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma.

Hoja kuu iliyojitokeza ni msisitizo zaidi kwa kwamba sekta ya habari inahitaji kujengwa katika misingi ya weledi, uwajibikaji na uaminifu ili kuendana na mahitaji ya upatikanaji wa taarifa sahihi kidigitali.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement