moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema

Waandishi wa habari wanawake wamehimizwa kutumia vyema kalamu zao kama daraja la kuunganisha changamoto za wananchi na Serikali, ili kusaidia utatuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii.

Rai hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, alipofungua Kongamano la kwanza la Malikia wa Habari.

"Tunatambua mchango wa wanahabari wanawake ni mkubwa katika kushughulikia changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili jamii na hususan kundi la wanawake," amesema.

Sambamba na hilo, Waziri Kairuki amesisitiza umuhimu wa wanahabari hao kusimamia kikamilifu vikundi na vyama wanavyoanzisha ili viweze kuleta matokeo chanya kwa wanachama na jamii nzima.

"Kuna fursa nyingi, tasnia ya habari na mawasiliano ambazo wanawake mnapaswa kuzichangamkia na Serikali ipo tayari kushirikiana nanyi, kuhakikisha mnazifikia,".

Amehimiza pia, ni muhimu wa umoja kwa waandishi wa habari wanawake wote waliopata ithibati, ili kurahisisha utambuzi wao rasmi Serikalini.

Mratibu wa Kongamano hilo, Penina Malundo, amesema lengo kuu ni kuwaleta pamoja waandishi wa habari wanawake ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuinua sauti yao kwa pamoja.

Lengo jingine ni kushirikiana katika shughuli za kijamii ili kila mmoja aweze kufikia malengo na kutimiza ndoto alizonazo.

Awali katika mdahalo, Mhariri wa Habari za Siasa kutoka gazeti la Mwananchi, Lilian Timbuka, alisema ni muhimu wa kujenga utamaduni wa kujitafutia maarifa mapya badala ya kusubiri mafunzo rasmi.

Mhariri Mkuu wa Clouds Media, Joyce Shebe, amesisitiza umuhimu wa wanawake kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na taarifa hasi zinazosambaa mitandaoni.

Mhariri wa Habari wa Gazeti la Tanzania Leo, Mary Geofrey, amesema kupitia kongamano hilo wamepata fursa ya kujadili na kueleza changamoto zinazowakabili pamoja na kubadilishana uzoefu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement