Kwa miaka saba mfululizo mchango wa Dkt. Rasha Kelej katika kuleta mabadiliko chanya kwa sekta ya afya na uwezeshaji wanawake na wasichana Barani Afrika umetambuliwa kimataifa.
Jarida la New African la Uingereza, wamemtambua tena Dkt. Rasha katika orodha “Waafrika 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Zaidi 2025”, sambamba na Marais wa Angola João Lourenço, Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Ghana John Mahama.
Ndani ya tamko la Merck Foundation kwa vyombo vya habari Dkt. Rasha ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Merck Foundation, ametambuliwa kwa mwaka wa saba mfululizo.
Orodha hiyo ya Waafrika 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Zaidi 2025 inajumuisha viongozi mashuhuri wa Kiafrika kutoka sekta mbalimbali kama vile ofisi za umma, biashara, teknolojia, wabadilishaji jamii, wanafikra na waunda maoni, ubunifu na michezo, wanaoathiri jamii na sekta zao kupitia kazi zao za kuhamasisha.
Orodha hiyo ilitolewa Desemba 22, 2025 Dkt. Rasha pia ni Rais wa Kampeni ya “More Than a Mother”, toleo hili maalum linaangazia watu wanaounda sasa na mustakabali wa Afrika. Waandishi na washirika wa jarida hilo wamepitia bara zima la Afrika kutambua kazi zao na mchango wao katika kuleta mabadiliko chanya ndani ya Afrika na kwengineko.
Akizungumza kuhusu utambuzi huo, Seneta Dkt. Rasha amesema “Nimepokea kwa heshima kubwa sana kutambuliwa kama mmoja wa Waafrika 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Zaidi na New African (Uingereza), na kutajwa pamoja na viongozi mashuhuri wa bara letu, wakiwemo Marais wa Angola, Ghana na Afrika Kusini, pamoja na wabadilishaji jamii wengine wengi. Nawapongeza wote.”
Amesisitiza "Utambuzi huu ni wa kipekee sana kwangu, kwani unatambua juhudi zangu endelevu za kujenga na kuimarisha uwezo wa huduma za afya, kuwawezesha wanawake wanaoishi na changamoto ya ugumba, na kuunga mkono elimu ya wasichana kupitia programu za Merck Foundation. Unanitia moyo mimi na timu yangu kuongeza dhamira yetu ya kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya kuleta athari endelevu na yenye usawa barani Afrika kwa vizazi vijavyo.”
Chini ya uongozi wa Dkt. Rasha Merck Foundation imekuwa ikiendesha programu zenye athari kubwa kama vile “Mpango wa Ufadhili wa Masomo kwa Watoa Huduma za Afya” ili kubadilisha mazingira ya huduma kwa wagonjwa na kuboresha upatikanaji wa huduma bora na zenye usawa za afya barani Afrika na kwingineko.
Harakati yao maarufu ya “More Than a Mother” aliyoiunda mwaka 2015 ili kujenga uwezo wa huduma za Uzazi na Tiba ya Ugumba, kuvunja unyanyapaa wa ugumba, kuongeza uelewa kuhusu kinga ya ugumba na ugumba wa wanaume, na kuunga mkono elimu ya wasichana; pamoja na programu ya “Educating Linda” inayosaidia elimu ya wasichana.
Katika kipindi cha miaka 13 iliyopita, Dkt. Rasha amefanya kazi kwa karibu na zaidi ya Wake wa Marais wa Afrika na Asia 33 kama Mabalozi wa Merck Foundation “More Than a Mother” katika nchi zao, kuongoza programu zao na washirika wakuu wakiwemo Wizara za Afya, Habari, Elimu na Jinsia, Taasisi za Elimu ya Juu, Watunga Sera, Jumuiya za Kimataifa za Tiba ya Uzazi, Vyombo vya Habari na Sanaa kutoka zaidi ya nchi 52.
“Ninafuraha kusema, tumetoa ufadhili wa masomo 2,500 kwa watoa huduma za afya kutoka nchi 52, katika taaluma 44 muhimu na zenye uhaba mkubwa. Najivunia kuwa wahitimu wetu wengi wamekuwa, au wako njiani kuwa, wataalamu wa kwanza katika nchi zao. Tunajenga urithi wa kudumu barani Afrika,” ameongeza.
Kupitia kampeni ya “Merck Foundation More Than a Mother”, ambayo ni harakati madhubuti inayolenga kuwawezesha wanawake wasio na watoto au wenye changamoto ya ugumba kupitia upatikanaji wa taarifa, elimu, huduma za afya na mabadiliko ya mtazamo, Dkt. Kelej amefanya kazi kwa karibu na washirika kuleta mabadiliko ya kijamii na kubadilisha mazingira ya huduma za uzazi na afya ya wanawake katika afya ya umma katika nchi 42 za Afrika na Asia.
“Kati ya ufadhili wa masomo 2,500 tuliyotoa, 770 ni kwa watoa huduma za afya kutoka nchi 42 kwa mafunzo ya kitabibu ya huduma za uzazi na Embryology, Diploma ya Uzamili ya mwaka mmoja na Shahada ya Uzamili ya miaka miwili katika Tiba ya Afya ya Uzazi na Ngono, Saikolojia ya Kliniki.
"Afya ya Wanawake, Bioteknolojia ya Uzazi wa Kusaidiwa kwa Binadamu na Embryology, Urolojia, Ujuzi wa Upasuaji wa Laparoscopy na Tiba ya Familia. Wataalamu hawa ni muhimu katika kuendeleza huduma bora na zenye usawa za afya ya wanawake kwa ujumla na afya ya uzazi na ugumba kwa ujumla,” ameeleza Seneta Rasha.
Aidha, Merck Foundation pia imekuwa ikiunga mkono wanawake wasio na watoto kwa kuwasaidia kuanzisha biashara ndogo ndogo kupitia programu ya “Empowering Berna”.
“Yote ni kuhusu kumpa kila mwanamke heshima na msaada anaostahili ili kuishi maisha yenye utimilifu, akiwa na mtoto au bila mtoto,” ameongeza.
Zaidi ya hayo, Dkt. Rasha ni mtetezi mkubwa wa elimu kama moja ya nguzo muhimu zaidi za uwezeshaji wa wanawake. Hivyo, kwa ushirikiano na Wake wa Marais wa Afrika, Merck Foundation hadi sasa imetoa zaidi ya ufadhili wa masomo ya kila mwaka 1,200 kwa wasichana wa Kiafrika wanaofanya vizuri kielimu lakini wanaotoka familia zisizo na uwezo, kutoka nchi 19 kuwawezesha kukamilisha masomo yao na kufikia ndoto zao.
Nchi hizo ni pamoja na Botswana, Burundi, Cabo Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon, Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Namibia, Nigeria, São Tomé and PrÃncipe, Tanzania, Togo, Zambia, Zimbabwe na nyinginezo.
Dkt. Rasha ni kinara na mwanzilishi wa mabadiliko ambaye maono na kujitolea kwake kumeleta mabadiliko ya maisha ya watu wengi barani Afrika.
Anasifiwa kwa juhudi zake za ubunifu zinazokabiliana na changamoto kubwa za kijamii na kiafya barani humo kama vile kuvunja unyanyapaa wa ugumba, kuunga mkono elimu ya wasichana, kukomesha ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia na ukeketaji wa wanawake, na kuendeleza uwezeshaji wa wanawake.
Kupitia uongozi wake wa kipekee, Dkt. Rasha ameunganisha vyombo vya habari, mitindo na sanaa kuwa sauti ya wasio na sauti. Mipango yake ya kipekee ikiwemo kipindi cha Televisheni cha Pan-Afrika, Mafunzo kwa Vyombo vya Habari kuhusu Afya, Tuzo za Mwaka kwa vyombo bora vya habari, wimbo, ubunifu wa mitindo na filamu, nyimbo za uhamasishaji, vitabu vya hadithi kwa watoto na filamu za uhuishaji, vimeleta mabadiliko ya kiutamaduni katika jamii.
Akiwa kiongozi wa maono ya mbali, Dkt. Rasha anahamasisha na kuelimisha zaidi ya wafuasi milioni 8.5 kwenye mitandao ya kijamii, akiwaweka karibu kupitia maudhui ya uwezeshaji na uhamasishaji. Kujitolea kwake bila kuchoka, mbinu zake za ubunifu, na shauku yake isiyoyumba vinaendelea kubadilisha mazingira ya kijamii na kiafya, na kuacha urithi wa matumaini, uwezeshaji na maendeleo barani Afrika.





Chapisha Maoni