moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Ule mvunjiko alioupata katika mguu wake na kulazimu alazwe hospitalini kutibiwa, ndiyo kipindi ‘ilipandwa mbegu’ ya u-daktari ndani ya moyo wake.

Kabla ya tukio hilo alikuwa ana ndoto aje kuwa mwalimu ili afundishe watoto, kwa sababu alikuwa anapenda mno kuwa karibu nao.

“[Lakini sasa] nilijiambia mimi nitakuwa daktari na nikaanza kujitambulisha kwa watu na marafiki zangu naitwa ‘doctor’ Tuni’,”.

Ujasiri ukaingia ndani zaidi ya kilindi cha moyo wake, akivutiwa kwa namna ambavyo daktari raia wa kigeni kutoka nchini Sweden alivyokuwa akimpatia huduma.

Alikuwa mkarimu kwake, mchangamfu alimpenda, unajua nini? … alimpa huduma mithili ya rafiki yake wa karibu aliyejuana naye siku nyingi, kumbe la hasha!.

Ni mgonjwa tu aliyefikishwa punde hospitalini, huu ni mkasa halisi simulizi yake Zaitun Bokhary.

Ukilitaja jina lake si geni sana maskioni mwa walio wengi hasa wale ambao kwa namna moja au nyingine, wamewahi kupatiwa huduma na mwanamama huyu.

Miongoni mwa madaktari wanawake wachache, mabingwa wa upasuaji hasa kwa upande wa watoto, ambao Tanzania inajivunia hivi sasa.

Zaitun ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa watoto [‘Pediatric Surgeon’], Hospitali ya Taifa Muhimbili [MNH].

Hivi sasa pia ndiye Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania [MEWATA] akitazamwa na kundi kubwa la madaktari vijana [wasichana] wanaochipukia nchini.

Kwa wenzetu wazungu wanasema ‘role model’ ambaye wengi wanajifunza kupitia yeye, ili siku moja nao wafikie ndoto na malengo yao wakilitumia Taifa.

Lakini haikuwa jambo rahisi kwa Dkt. Tuni kufikia hatua hiyo ndani ya makala haya utasoma visa na mikasa aliyopitia ambayo hata hivyo hakuruhusu imkatishe tamaa na kuvunja nia yake ya ndani.

NI KAZI YA WANAUME

Enzi za mababu na mabibi zetu, dhana potofu nyingi zilikuwapo iliaminiwa na kundi kubwa la watu kwamba u-daktari ni taaluma ya wanaume zaidi na si wanawake.

Hiki kilikuwa kigingi cha kwanza alichokumbana nacho tangu alipoanza kuwajuza watu nia yake ya kutaka kusomea taaluma hiyo.

“Nilipotibiwa na yule daktari wa Sweden nilipenda mno namna alivyonihudumia, ilinifanya nifikiri zaidi [u-daktari] hii ni kitu kizuri [kazi / taaluma nzuri],” anasimulia.

Anaongeza “Tukiwa hospitalini kwanza tunacheza, kisha ananiuliza namna ninavyohisi ile ilinifanya nianze kujikuta napenda u-daktari na ndipo nikaanza kujiita ‘dokta’ Tuni.

Anasema alitibiwa na kupona wakarejea nyumbani akiwa amebeba nia yake ya kuwa daktari siku moja katika maisha yake asaidie kuokoa maisha ya wengine wenye matatizo mbalimbali.

‘MONITOR MDOGO’

Ujasiri aliokuwa nao katika umri wake mdogo licha ya kuwa na umbile dogo kuliko wenzake, anakumbuka akiwa darasa la kwanza, ndiyo kwanza siku ya kwanza amejiunga shuleni alichaguliwa kuwa ‘monitor’.

Ndiyo aliaminiwa na kupewa uongozi wa dada wa darasa lake, ni kati ya siku muhimu kwenye maisha yake anayoikumbuka vema.

“Kila siku niliamini [na ninaamini] nimezaliwa kuwa kiongozi,” anasema na kusimulia zaidi,

“Nilipoanza darasa la kwanza, siku ya kwanza, nilikuwa ‘mdogo’ [yaani nina] umbo dogo [kuliko wengine], mwalimu wetu alisema inatakiwa darasa lipate ‘monitor’.

“[Sasa] watu wananyoosha mikono, mimi mwalimu hanioni [kwa vile nilikuwa mdogo], niliinuka na kwenda moja kwa moja hadi mbele kwa mwalimu.

Anaongeza “Nikiwa nimenyoosha mkono mbele yake, nikamwambia nataka kuwa ‘monitor’.

“Mwalimu akasema ‘okay’ Zaitun atakuwa ‘monitor’ wetu,” anasema alikuwa kiongozi wa darasa lao jambo ambalo alilifurahia.

SAYANSI ACHANA NAYO

Alifanikiwa kuhitimu darasa la saba na akaendelea na masomo ya sekondari, akiwa huko bado aliendelea kuamini atakuwa daktari.

 “Siku ya kwanza nilipofika sekondari niliuliza tena ili niwe daktari natakiwa kusoma masomo gani?

“Nikaambiwa lazima masomo ya sayansi lakini masomo hayo ni ya wanaume,” anasimulia.

Dkt. Zaitun anasema amekuwa katika dhana hiyo potofu ambayo iligubika jamii yake iliyomzunguka lakini hakukubali kurudi nyuma na kukata tamaa.

“[Kuna marafiki zangu wengi walikuwa wananiambia] Zaitun usifanye hiki ni cha wanaume, [hata] ukiuliza maoni kwa wengine [waliendelea kuniambia u-daktari] ni kazi ya wanaume.

NANI KAMA MAMA?

Licha ya maoni hayo ya kukatisha tamaa, Dkt. Zaitun anasema alikuwa na mwanamke jasiri na shupavu nyuma yake.

Ni mwanamke huyo ambaye kila alipomfikia na kumueleza nia yake tangu siku ya kwanza hakusita kumwambia INAWEZEKANA.

“Siku zote namkumbuka mama yangu, baba yetu alituacha [alifariki] tukiwa wadogo mimi na kaka yangu.

“[Hivyo] mama yangu [katika safari yangu] alikuwa kila kitu kwangu,” anasema huku akitabasamu.

Anaongeza “Mama alikuwa ananiambia akiniangalia tu [namna nilivyo] anaona tayari mimi ni daktari.

“Kwa hiyo mama kasema nani atabisha?! Hivyo nilikuwa napenda sana kusoma, nilikuwa nasoma kwa bidii na nilifanya vizuri [darasani].

“Nilipenda pia kusoma novel [riwaya], ya kwanza ilikuwa ni ‘A Women of Substance’, ni kitabu kizuri mno.

Anasema kitabu hicho kinamuelezea mwanamke kwamba ni kiumbe mwenye nguvu, ushawishi na mchapakazi.

“[Mwanamke] ni ‘positive influence’, nilipokisoma kile kitabu nilienda kuwasimulia wenzangu ili nao wakisome, ila sasa [kusoma au la] kila mtu na ‘interest’ yake.

“[Binafsi] nikawa nasoma vitu vingi katika umri wangu mdogo,” anasimulia, hii nayo ni siri yake iliyompa maarifa mengi na ujasiri wa kusonga mbele zaidi.

U-DAKTARI HALISI

Anasema alifanikiwa kuhitimu sekondari akifanya vizuri katika masomo ya sayansi akaenda chuo na kusoma rasmi taaluma ya u-daktari.

 “Baada ya kuhitimu ‘degree’ yangu ya kwanza, nikaenda ‘internship’ [mafunzo kwa vitendo] Mbeya Zonal Regional Hospital [MZRH],”.

Dkt. Zaitun anadokeza tangu awali alikuwa anataka kuwa daktari bingwa wa watoto lakini akiwa pale siku ya kwanza alikutana tena ile dhana hasi kwamba mwanamke hawezi kuwa daktari.

“Kule Mbeya [kipindi hicho] walikuwa wanaamini pia mwanaume peke yake ndiye anaweza kuwa daktari.

“Kwa hiyo sisi tukiwa pale tulikuwa tunaitwa ‘ma-nesi’ [wauguzi], nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu mmoja yeye alikuwa anakasirika sana kuitwa nesi.

“Alikuwa anakereka mpaka anapata ‘stress’, nikawa namwambia ‘why’ kwani atabadilika [kuwa nesi?] hapana, nikamwambia awe na furaha,” anasimulia.

Anaongeza “.., nilimwambia itabadilika [hiyo dhana] taratibu,”. Anazikumbuka pia nyakati ngumu za kutokukubaliwa na baadhi ya viongozi wake.

“Nilikuwa ‘smart’ nilikuwa navaa kiatu kirefu hata nikiwa ‘round’ [kuwapa huduma wagonjwa wodini].

“Kwa sababu nilizoea tangu nikiwa masomoni. Hata leo nikivaa ‘flat’ naona nashindwa kutembea.

 Anasimulia zaidi, “Kuna kiongozi mmoja alikuwa ananichukulia kwamba naringa, alikuwa anasema hajawahi kuona daktari anavaa ‘high hills’.

“Alisema siwezi kuwa daktari nitaishia tu nilipokuwa, alikuwa hanikubali kabisa, nikaendelea kufanya kazi kwa bidii kubwa.

“Kibaya nilikuwa na-m-prove wrong’ kwamba wanawake anaowachukia wanaweza kufanya vizuri kuliko anavyofikiria, nilifanya kazi vizuri sana,” anasema.

TIBA UPASUAJI

Anasema ilifika muda wa kuwa katika kitengo cha upasuaji, aliyekuwa kiongozi wa hapo ndiye aliyempa morali ya kugeukia na kujikita zaidi katika eneo hilo.

“Lakini lilikuwa ni eneo gumu zaidi, kwa sehemu kubwa ‘surgeons’ walikuwa wanaume. Nilivyofika pale yule ‘head of department alini-impress’ sana.

“[Namna] alivyokuwa ‘anani-treat’ [nilipenda mno], kuna siku aliletwa mtoto mdogo na tatizo kubwa la kupasuka kwa appendix,”.

Anasema mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka 10 alionekana mwenye maumivu mengi na makali kwa tatizo lililokuwa linamkabili.

“Nilipata huzuni, kuona mtoto mdogo kiasi kile anaumwa namna ile, walichelewa kumleta hospitali kupatiwa matibabu ikafikia hali mbaya namna ile.

“Nilikuwa ‘on call doctor’ siku ile, nikampigia ‘head’ akaniambia mtoto apelekwe 'theater', yeye akaja na tukampatia matibabu.

Anaongeza “Mtoto baada ya ‘surgery’ siku ya pili alibadilika kabisa [aliendelea vizuri mno], mpaka akapewa ruhusa kurudi nyumbani.

“Kile kitu kilinifanya niipende ‘surgery’, yule daktati alikuwa ananipa moyo ‘Dkt. Zaitun’ upo vizuri.

“[Nikawa najisemea] ananipa moyo tu, ila alinifanya nipende nilichofanya, mwisho nikasema nataka niwe ‘surgeon’.

WALINISHANGAA

Anasema baadae ndipo akajiunga na MNH huko nako akakuta wanaume ndiyo wengi kwenye eneo hilo kuliko wanawake.

Anasema wanawake aliowakuta ‘surgeon’ MNH walikuwa wanne tu kipindi hicho, alipowaambia marafiki zake anataka kuwa surgeon walimwambia asithubutu, atachelewa kupata mafanikio.

“Waliniambia nitapoteza muda, nitachelewa, nikamuuliza tena mama yangu akaniambia ‘unaweza kufanya, kwanini ushinwe kama kuna walioweza’,” anasimulia.

Dkt. Zaitun anaongeza “Nikasema sawa, nikaomba nipangwe nikafanya ‘surgery’ walishangaa.

“[Unajua kipindi kile] wanawake walikuwa wanakimbia [hawapo tayari kuwasurgeon], nilifanywa kuwa ‘register’ na nikafanya vizuri.

“[Baadae] nilienda KCMC kusoma tena kuna Profesa alikuja na huyo ndiye akawa ‘role model’ wangu mpaka leo,” anasema na kuongeza,

“Aliniambia mimi ni ‘surgeon’ mzuri, alinishauri nijikite zaidi katika pediatric surgeon itanipendeza sana.

“Nikasema itanifaa kwa sababu nitakuwa karibu na watoto kwa sababu nawapenda sana [kumbuka awali nilitaka kuwa mwalimu nikiamini nitakuwa karibu na watoto, nicheze nao na kuwafundisha.

“Nikawa daktari, baadae nikaenda Misri kwa masomo zaidi kwa miaka mitatu,” anasimulia Dkt. Zaitun.

Pamoja na u-daktari bingwa, Zaitun ni mke wa mhandisi, mama wa watoto wawili waliopo vyuoni hivi sasa.

Mmoja akisomea masuala ya ‘marketing and business administration’ na mwingine akisomea ‘clinic physiochology’.

MWANAMKE UNAWEZA

Simulizi yake aliitoa alipozungumza katika tukio la ‘BINTI KAIRUKI’ akiwapa maarifa wasichana na wanawake waliopo katika Chuo Kikuu cha Afya Hurbert Kairuki, Dar es Salaam.

Tukio hilo liliandaliwa na Serikali ya wanafunzi katika chuo hicho [KUSA], ilikuwa kivutio cha wengi siku hiyo wakionesha wazi ilikuwa inawapa mafunzo yatakayowasaidia katika safari yao..

“Naamini kila mwanamke ni ‘multi task’, yaani tunaweza kufanya mambo mengi na kila kitu kikaenda sawa sawa kama ulivyopanga,” anasisitiza.

Anaongeza “[Jambo muhimu] hakikisha unajiamini wewe binafsi kwanza, jenga ufahamu wako kwamba unaweza.

“Pia ni vema kuchagua ‘mentor’ wako mzuri mapema, siyo unakaa unasubiri mpaka umalize chuo ndiyo utafute ‘mentor’ wa kukuongoza.

“Tafuta ‘mentor’ tangu sasa unavyosoma [chuoni], kama mlivyofanya [mimi tangu awali], leo [hiki mlichofanya, kuandaa ‘BINTI KAIRUKI’ ni kitu kizuri na kikubwa,”.

‘STUDENT CHAPTER’

Anadokeza “MEWATA tunachofanya sasa tumefungua ‘student chapter’ ambayo wengi [wenu] mpo [humo] na inafanya vizuri sana.

“[Viongozi wenu] ‘wana-organize event’ mbalimbali, inasaidia mno kuwajenga kwa sababu ili] , uwe kiongozi mzuri unatakiwa kuanzia huku chini,”.

“Huwezi kuwa kiongozi juu tu, [mimi] nilianza kujitolea [miaka mingi katika MEWATA] tunaenda kufanya ‘screening’ chini ya Dkt, Malina Njelekela.

Anaongeza “Lindi, tumetembea karibu mikoa yote ya Tanzania, nyakati zingine unajilipia nauli mwenyewe.

“[Ni ishu] kuna muda kila mtu anataka awe ‘sponsored’ unalipiwa na nani, ila ukijilipia ukaenda [kule] unajifunza.

“Hata ‘meeting’ kama hii zungumza unachofikiri, [lakini] unakaa kimya ila ukitoka nje unasema ulikuwa na ushauri ila ukajisikia aibu, [ukiongea] ndipo unapoanza kujijenga.

Anasisitiza “Ongea leo, kesho mwisho utajikuta [wengine] ‘wanaku-note’ ukisimama kuongea [wanaona] una ‘point’, inachukuliwa na wengi.

TUNAPIGA HATUA

 “Mimi ni ‘pediatric surgeon’, sasa najivunia tulipo ni pazuri si kama [ilivyokuwa] kwanza [pediatric surgeon] ilikuwa haijulikani.

“Ukizungumzia ‘surgery’ ilitazamwa ni kwa ajili ya watu wazima, lakini sasa kuna ‘pediatric surgery’, nayo inajulikana, inajitegemea.

Anasema sasa ndani ya Muhimbili kuna ‘theatre’ nzuri kwa ajili ya watoto, walipata washirika kutoka nje ya nchi wakafanikisha ujenzi huo kwa pamoja.

“Leo huduma zipo nzuri, kwa siku tunafanya upasuaji kutibu watoto, hawahitaji tena kusubiri muda mrefu,”..

Anaongeza “Tukaanza ushirikiano na Saudi Arabia, Ujerumani sasa tuna makubaliano wanafunzi wetu wanaofanya ‘super specialization’ wanaenda Ujerumani.

“Wanajifunza mengi ikiwamo ‘altitude’, wanaona ‘quality doctor’ anatakiwa ‘ku-behave’ namna gani.

“.., siyo unaongea na mgonjwa na unataka kujionesha wewe ni nani,” anawapa somo mabinti hao.

‘PANUA FIKRA’

Anawashauri wasiogope kujiunga na vyama vya kitaaluma ndani na nje ya nchi kwani ni fursa nzuri ya kupanua fikra zao pamoja na kupata fursa pana zaidi katika sekta.

“Mimi nimejiunga na ‘association’ mbalimbali za kimataifa, niliwahi pia kuchaguliwa kiongozi wa madaktari chini ya miaka 40 Afrika.

“Unatakiwa kufikiria mbali zaidi kidunia, si tu kwa Tanzania pekee, nipo [umoja wa] ‘global surgery’ ni mpango wa ki-dunia.

“Uongozi wa ‘under’ 40 niliupata kwa kuteuliwa tukiwa mkutano wetu wa Ghana, walijadili wakanichagua mimi kuwa ‘country co-ordinator’.

Anasisitiza “Tukiwa na mashirikiano haya kunakuwa na hizi ‘exchange program’ nyingi, madaktari wao wanakuja na wa kwetu wanaenda nje kujifunza.

“[Fursa hizi] zinasaidia kukutengenezea ‘confidance’ ukifika unatengeneza ‘network’ na ‘partinaship’.

Anaongeza “Sasa siyo ukipata na kwenda unasema umeenda tu kuiwakisha Kairuki, tafuta ‘network’ yako.

“Unatengeneza ‘collabotarion’ ukirudi [nchini unaendelea kufanya nao kazi], ni kitu nashauri, ianzie kwako, utafanikiwa … vinginevyo utakuwa tu unasema mbona fulani anaenda nje [mara nyingi].

“[Nje] huendi hivi hivi, kuna ‘conference’, unaambiwa tuma ‘abstract’ na hapa nchini ‘cases’ mnazo tena kule ni zinazohitaji.

Anabainisha “Hawapati [kama za huku kwetu] kwa mfano sisi [Muhimbili] kuanzia Januari mpaka sasa hivi tuna zaidi ya kesi sita ambazo ni ‘very interesting’.

“Hizo ni kwa mwaka huu tu, sijasema kuhusu za miaka mingine ya nyuma, tumeshazichapa kwenye majukwaa ya kitaaluma ya kimataifa.

“Mikutano ya kimataifa ipo mingi, mimi nilianza kwenda kwa kujilipia mwenyewe leo hii napata 'full sponsorship' naenda,” anawapa mfano halisi.

Pamoja na hayo, anawahimiza pia kutumia vema majukwaa ya mtandaoni na si kwa mambo yasiyofaa zaidi katika maisha yao.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement