moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Kijana mdogo anayeugua magonjwa kama moyo, kisuakari, shinikizo la damu, saratani na mengineyo ilikuwa jambo la nadra mno kulikuta ndani ya jamii, miaka ya zamani.

Enzi hizo ilikuwa jambo la nadra pia kupata mtoto/watoto wamezaliwa na wanaishi na magonjwa hayo, Tanzania.

Magonjwa Yasiyoambukiza [NCDs] yalitafsiriwa ni ya watu wazima zaidi lakini miaka ilivyosonga mbele, hali ilionekana kubadilika.

Vijana na watoto nao wakaanza kuugua magonjwa hayo na kasi yake ikaongezeka kiasi cha kugeuka kuwa  tishio kubwa la ki-afya.

“Kipindi kile ukisikia mtu ana ugonjwa wa moyo yaani ni mtu mzima sana na umri umeenda sana, tofauti na sasa naona eti watoto nao wanaugua moyo,”.

Ni kauli yake Elishaza Kidau alipozungumza na M24 TANZANIA MEDIA katika mahojiano haya maalum.

Anasema kipindi cha miaka ya zamani watu walikula zaidi vyakula vya asili tofauti na sasa watu wanapenda zaidi vyakula vya kisasa.

Ana umri wa miaka 53, Mkazi wa Tabata ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam anasema kuna uhitaji mkubwa ndani ya jamii kuhusu elimu ya lishe, ulaji na mtindo bora wa maisha kwa ujumla.

AGENDA MKAKATI

Miaka 10 iliyopita wataalamu wa kada mbalimbali waliketi pamoja na kuangazia kwa kina juu ya janga la NCDs ndani ya jamii ya Tanzania.

“Changamoto kubwa ilikuwa ukuaji/ongezeko la NCDs. [Tafiti unaonesha mwaka] 2012 yalionesha yanakuwa kwa kasi,”.

Anasema hayo na Meneja Miradi wa TANCDA Happy Nchimbi katika mahojiano maalum na M24 TANZANIA MEDIA.

Anaongeza “[Ugonjwa wa] kisukari [ulikuwa] 9%, Shinikizo la damu 26%, saratani, na sasa kuna changamoto ya magonjwa ya afya ya akili.

“Tuliona umuhimu wa kuunda muungano huo, wizara pia tumeziunganisha ili kila mmoja ashiriki katika mapambano haya.

Anasema kikubwa ambacho walibaini ni uelewa duni uliopo ndani ya jamii kuhusu NCDs.

“[Kulikuwa nab ado kuna] imani potofu [katika jamii] pale mtu akipata/anapopata magonjwa haya,” anasema.

Anasema bado kuna ambao wanaamini chanzo ni imani potofu nah ii inadhihirisha wazi pamoja na hatua ambazo zimepigwa katika kuyakabili kuna uhitaji wa elimu endelevu.

HATUA ZIPI ZIMEPIGWA?

Unaweza kuwa unajiuliza ikiwa miaka 10 imefika tangu TANCDA imenzishwa, pengine ni hatua gani ambazo Tanzania imeweza kupiga katika mapambano hayo.

Je, mapambano haya yanatoa taswira gani kwa Tanzania siku zijazo licha ya kuendelea kuwapo changamoto hiyo ya uelewa duni.

“Taswira unayoipata sasa hivi ya mapambano dhidi ya NCDs [kwanza] neno lenyewe Magonjwa Yasiyoambukiza ilikuwa changamoto kutamkwa [siku za nyuma],”.

Anasema Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Afya ya Akili na Ajali wa Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu.

Anafafanua zaidi “Lakini miaka ya sasa utaona watu wanafanya mazoezi kama jogging, hawafanyi tu mazoezi.., wanasema wanafanya ili kujikinga dhidi ya NCDs.

“Unaona uelewa katika jamii umeanza kuongezeka [japo ni kidogo], katika miaka 10 tuliyonayo na TANCDA, wamekuwa sehemu kubwa sana kama kioo cha kuhamasisha jamii.

“[Ikiwamo] kuhamasisha vyama [vingine vya Magonjwa Yasiyoambukiza], kuhamasisha asasi za kiraia na watu wanaoishi na NCDs katika jamii katika kupeleka ule ujumbe/elimu ndani ya jamii,”.

Anasisitiza [Hivyo] limekuwa jambo la msingi sana kwetu katika eneo la kuhamasisha elimu kwa jamii.

MAFUNZO YA KINA

Dkt. Ubuguyu anasema TANCDA imeshirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI katika kuwapatia elimu watumishi wa afya.

“Kwa mfano katika miaka miwili iliyopita tuliweza kutoa mafunzo kwa takriban watumishi 3,000 katika hospitali 710 hasa vituo vya afya nchi nzima.

“Lengo ni kuhakikisha katika ngazi hiyo huduma zinatolewa, tuliandaa mikakati pamoja iliyotusaidia kutafuta wadau na washirika ili kufanikisha hilo.

Anasema pamoja na mafunzo, TANCDA imeshirikiana na Serikali katika eneo la vifaa tiba na baadhi ya dawa za wagonjwa.

“Ili wagonjwa watakaogundulika wapate matibabu, mchango wa TANCDA si mdogo katika ‘vita’ dhidi ya NCDs,” anasema.

TAFITI ZA NCDs

Je, Tanzania imenufaikaje na TANCDA katika eneo la tafiti za magonjwa hayo ambayo yanaathiri idadi kubwa ya raia wake hivi sasa.

“Upande wa tafiti mimi ni mmoja wa wanufaika, katika kipindi cha miaka 3 iliyopita wameweza kufadhili PHd karibu 5,” anasema.

Anaongeza “‘Masters’ 10 na ‘undergraduate degree’ ya 1 watu 20, miaka 3 mfululizo wameweza kufadhili mashindano ya ubunifu na tafiti kwa ajili ya vyuo vikuu nchini.

“Tumepata watu wengi na bunifu nyingi zimezalishwa huko na tumetengeneza pamoja mkakati wa tafiti katika NCDs na zipo tafiti nyingi ambazo tumefanya kwa pamoja.

“Wizara ya Afya, NIMR tunafanya kazi katika eneo hili. Hata sasa kuna tafiti zaidi ya 5 wanashiriki ama kututafutia wafadhili au wao wenyewe kufadhili tafiti hizo,”.

Anasisitiza “Upo unaofanyika bado matokeo hayajatoka ni mkubwa wa kitaifa [step survey] WHO inakuwa kiongozi wa juu katika kufadhili ila kuna baadhi ya maeneo TANCDA inafadhili.

“Kuna tafiti nyingine kubwa wanashiriki moja kwa moja na kuna za kuangalia matokeo ya matibabu hasa kwenye kisukari aina ya 1 na kinachowakuta watu wazima,” anasema.

Anabainisha wapo wataalamu wengine wanaotafiti kuhusu saratani, wanapata fedha kutoka kwa TANCDA.

JE WANAFIKIA LENGO?

Kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa [UN] anatakiwa kufikia Malengo Endelevu [SDGs] yaliyowekwa ifikapo 2030.

Je kwa upande wa mapambano dhidi ya NCDs kwa tathmini yao wanaona Tanzania imefikia hatua gani kufikia hasa lengo namba 3 la SDGs linalohimiza Afya kwa Wote.

“Kwa kiwango kikubwa tumesogea ukiangalia hakuna hata ‘indicator moja’ ambayo hatujaifanyia kazi,” anasema Dkt. Ubuguyu.

Anaongeza “Tumepiga hatua kubwa. Si mchango wa Wizara ya Afya na Serikali peke yake ni pamoja na wadau na TANCDA ndiye jumuiya shirikishi na wengine wote.

“Huu ndiyo mwamvuli, nashindwa kutaja wadau mmoja mmoja, [lakini] kwa angalau theluthi moja tumesogea kufikia malengo endelevu.

Anasema hizo hatua walizosogea mdau mkubwa aliyewashika mkono ni TANCDA.

“.., na wadau wengine, ikiwamo pia waandishi wa habari najua mpo ndani yake kupitia chama chenu.

GHARAMA ‘MTIHANI’

Suala la gharama za matibabu bado wanaitazama ni changamoto kubwa mno katika mapambano hayo.

“Ni changamoto hasa kwa wale wanaougua lina ugumu kwa mtu mmoja mmoja na jamii,” anasema na kuongeza..,

“Ndiyo maana mtaona Serikali hatua iliyochukua ni kuleta Bima ya Afya kwa Wote,”.

“[Kimsingi] hakuna nchi duniani ambayo Serikali yake itasema kwamba tumuhudumie kila mtu anayeugua NCDs.

“Kwenye bajeti ya ndani au sekta moja, moja, kwa hiyo tunatumia mkakati zaidi ya mmoja, kwanza kutenga bajeti maalum.

“Pili mfuko wa pamoja ambayo mara nyingi inakuwa mifuko ya bima na unaona inaenda hivyo.

“Tatu inakuwa ni wafadhili na TANCDA wanatusaidia eneo hili la tatu sana kuongea na wafadhili wengi hawaipi fedha serikali moja kwa moja wanawapa wadau.

Anasisitiza “Sehemu kubwa ya fedha za mafunzo TANCDA waliongea na wadau wakatupa fedha, kuna wanaotibiwa bure kisukari aina ya kwanza.

“‘Addressing’ ni TANCDA na akipokea analeta Serikalini,”.

MABADILIKO YA TABIA

Anasema mabadiliko ya tabia ili kuepukana na NCDs bado imeendelea kusalia changamoto katika ‘vita’ hiyo.

“Si nyepesi ni kama [tunavyoenda nyumba za ibada wanakemea] usiibe, usizini ni [suala la] mtu mmoja mmoja na tabia yake,” anafafanua.

Anaongeza “Sasa hii ni kufanya kampeni endelevu, ni eneo linahitaji gharama kubwa sana, ni ngumu kuzihesabu, mfano leo tulivyokutana hapa ni gharama imetumika.

“Tunapopata wadau kama TANCDA wanatusaidia, hili si rahisi kuingia kwenye bajeti ya Serikali ila ni rahisi kuingia kwenye bajeti za wadau,”.

TUTAENDELEZA USHIRIKIANO

Happy anasema miaka 10 ya TANCDA inatoa tafsiri chanya, kubwa na ushindi hasa katika kujenga ushirikiano madhubuti.

“TANCDA, Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI na wizara nyingine katika kupambana na NCDs,” anasema na kufafanua zaidi..,

“Tumeleta ushawishi mkubwa kwenye jamii, mashuleni na makundi mbalimbali juu ya kujikinga na NCDs.

“Tumejenga uelewa kwa waandishi wa habari nchi nzima kwa vyombo vya mtandaoni, magazeti, runinga na radio pia.

“Pia kuweza kuwakutanisha watu pamoja wanaoishi na magonjwa mbalimbali, wanaelimisha tuna walimu pia tunashirikiana nao katika hili,” anasema na kusisitiza wataendeleza zaidi mapambano.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement