moja

Responsive Advertisement


Dar es Salaam

Uwepo wa kimbunga kilichopewa jina 'CHIDO' umerekodiwa na kuripotiwa katika Bahari ya Hindi Kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imetoa taarifa ya tahadhari kwa wananchi juu ya uwepo wa kimbunga hicho.

TMA imeeleza maeneo ambako kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea ni huko kaskazini mwa Msumbiji.

"Katika kipindi cha siku nne zijazo [Des. 13 hadi 16, 2024]," taarifa hiyo imebainisha na kufafanua zaidi...

"Kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini. 

"Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga 'CHIDO' kinatarajiwa kupita [Kaskazini mwa Msumbiji] na maeneo ya kusini mwa nchi yetu,".

Imeelezwa upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa ambayo itaambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari.

"Kwa maeneo ya Mtwara na maeneo jirani hususan kati ya Des. 14 na 16, 2024," imedokezwa.

Ushauri umetolewa "Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka TMA pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta,".

TMA imesema inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement