moja

Responsive Advertisement

  

 

NA VERONICA MREMA – DAR ES SALAAM

KIBAIOLOJIA mtu mume na mke wanapoamua kuanza maisha ya pamoja, kulala pamoja ‘kinyumba’, wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wanatarajia kwamba ndani ya miaka miwili wawili hao wawe wameweza kupata mtoto au watoto.

Lakini iwapo muda huo unapita bila kuweza kusababisha mimba hapo hupata shaka kwamba huenda kuna tatizo ambalo limechangia hali hiyo.

Hapo huhitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tatizo na hatimaye kulipatia ufumbuzi ili waweze kupata mtoto, watoto katika maisha yao.

“Lakini bahati mbaya sana nchini mwetu watu bado hawana mwamko wa kutafuta tiba mapema kwa wataalamu huanzia kule kwenye tiba asili na mbadala, wengi hudhani wamerogwa.

“Matokeo yake hadi anakuja huku hospitalini, unakuta wengi tayari wamefikisha miaka sita na kuendelea, wakati mwingine unakuta tatizo limeshakuwa kubwa,” anasema Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Vincent Tarimo.

Dk. Tarimo anasema tatizo la wenza kushindwa kusababisha mimba na hatimaye kupata watoto ni kubwa nchini na kwamba linaonekana kuongezeka siku hadi siku.

 

“Binafsi, katika kliniki yangu ambayo huwa kila siku ya jumatano huwa naona si chini ya wagonjwa watano mpaka 10 ambao wanakabiwa na tatizo hili,” anabainisha.

Anaongeza “Katika Idara yetu kuna kliniki nne, kila daktari ana idadi ya wagonjwa wake anaowaona, sasa mimi peke yangu kwa siku ya jumatano pekee huwa naona hao watano mpaka 10, ni wengi.

KUZIBA MIRIJA

Dk. Tarimo anasema miongoni mwa wagonjwa wanaonwa hasa wanawake wengi wao shida kubwa inayowakabili ni kuharibika au kuziba kwa mirija ya uzazi.

“Kuna ugonjwa unaitwa endometriosis, wanawake wengi wanaokuja kliniki wanakabiliwa na ugonjwa huu, ni ugonjwa ambao unakuta huyu mama maumbile yake ni tofauti kidogo na wanawake wengine.

“Kwamba, unakuta ule ukuta unaotakiwa kuota ndani ya kizazi unakuwa umeota sehemu zingine ambazo ni nje ya kizazi, sasa kule zilipo kwa sababu zinakuwa chini ya ‘influence’ ya homoni ya estrogen.

“Kule (nje ya kizazi) zilipo, zinaota, zinavimba, kama kuna kitu chochote kikaja juu yake, unakuta vinafanya vinashikana, vinajaa hatimaye zinasababisha ile mirija ya uzazi kuvutwa na kushikamana,” anafafanua.

MAAMBUKIZI

“Shida nyingine ambayo inawakabili wanawake wengi ni maambukizi, siku hizi maisha yamebadilika si kama zamani, ambapo wasichana waliolewa pindi tu walipovunja ungo.

“Siku hizi unakuta wanakaa muda mrefu hawajaolewa, pengine kwa sababu wanakuwa masomoni, lakini wapo ambao huanza kushiriki ngono tangu wakiwa masomoni.

“Tatizo ni kwamba unakuta mwingine unakuta hana mpenzi mmoja, mpaka amalize chuo na hadi akaolewe unakuta tayari ameshiki ngono na wanaume wengi,” anasema.

Anaongeza “Katika hali ya namna hiyo ni rahisi mwanamke huyo kuwa amepata infections (maambukizi) mbalimbali, kitendo cha kushiriki ngono na wanaume wengi humuweka kwenye hatari.

 

NITAONGEZEEEEEAAAAAAAAA

 

UPANDIKIZAJI

Daktari huyo bingwa wa magonjwa ya wanawake anasema upandikizaji hufanyika baada ya kuwa wameotesha mimba kitaalamu kwa kuchukua yai kutoka kwa mama na mbegu kutoka kwa baba.

“Huwa tunavuna yai la mama na mbegu ya baba kisha tunaotesha kitaalamu kwenye kifaa maalum chini ya uangalizi wa darubini maalum.

“Hii ni njia hii ni ya mkato ili kuweza kuwasaidia (wenza) kupata mtoto au watoto kwa sababu pengine unakuta mirija ya mama imeziba, kwamba isiwe kwa sababu mirija yake imeziba basi amelaaniwa asipate mtoto, la hasha, inawezekana kupata mtoto.

“Hivyo, tunaotesha mtoto, kama mama anacho kizazi, tunakwenda kumpandikiza tumboni mwake, anaishi na hatimaye kuzaliwa,” anasisitiza Dk. Tarimo.

MBEGU DUNI

Anasema kwa upande wa wanaume zipo pia sababu mbalimbali ambazo huchangia wao kushindwa kutungisha mimba.

“Wapo ambao wanakabiliwa na shida ya kuziba kwa mirija, wengine mbegu zao hazitoshi, hafifu na wapo ambao huwa tunakuta hazina mikia,” anabainisha.

Anaongeza “Wakati mwingine huwa tunabaini wenza wote wanakabiliwa na tatizo na wakati mwingine huwa tunakuta mwenza mmoja ndiye mwenye tatizo, kama mwenza mmoja akiwa ndiye anakabiliwa na tatizo huwa rahisi zaidi kuwasaidia.

WENGI HUENDA NJE YA NCHI

Anasema Watanzania wengi wanaokabiliwa na tatizo la kukosa mimba huenda kutafuta msaada nje ya nchi hasa India, Kenya na Uganda.

“Tanzania tumechelewa mno kuanzisha huduma hii, tukijilinganisha nan chi nyingine katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya walianzisha zamani, Uganda nao wakafuata, wenzetu wapo mbali mno,” anasema.

Anaongeza “Japo hivi sasa huduma hii imeanza kutolewa kwenye hospitali binafsi, lakini tupo nyuma, ki-utaratibu, Muhimbili ni hospitali kubwa ya Taifa, ilipaswa kuwa imeanzisha huduma hii.

“Kwa sababu inategemewa kutoa mwongozo namna huduma hii itakavyotolewa nchini, sasa utaona hospitali binafsi zinatoa huduma hii lakini Muhimbili, hospitali ya Taifa hatuna, hii si sahihi,” anasema.

Anasema kwa msingi huo huu sasa ni muda mwafaka kwa Muhimbili kuanza kutoa huduma hiyo kwani tathmini inaonesha tatizo linazidi kuongezeka siku baada ya siku.

SERA NA MIONGOZO

Dk. Tarimo anasema ili kufanikisha huduma hiyo na kuifanya iwe endelevu zaidi inahitaji nchi kuwa na sera na miongozo madhubuti.

“Sera na miongozo ambayo nchi itatengeneza itafanya huduma iwe na manufaa zaidi, nchi za wenzetu wametunga sera katika makundi ya aina zipatazo mbili, wapo ambao Serikali zimeweka miongozo inayoruhusu mwanamke mwingine kuweza kubeba mimba ya mtu mwingine.

“Kuna tatizo la kibaiolojia, yaani unakuta mwanamke hana kabisa kizazi, anaishi na mume hawezi kushika mimba, lakini mayai yake yanafaa kwa upandikizaji, hivyo, yale mayai huvunwa kisha mbegu za mumewe nazo huvunwa.

“Baada ya kuyaotesha, huchukuliwa na kupandikizwa katika mji wa mimba wa mwanamke mwingine, ambaye huilea mpaka mtoto au watoto, watakapofikisha umri wa kuzaliwa,” anasema.

Anaongeza “Mara nyingi si rahisi mwanamke kujitambua kwamba hana kizazi, kimsingi kilema si lazima kiwe nje, wengine vipo ndani.

“Lakini kimaumbile ni mwanamke kabisa na anakuwa anaona siku zake kama kawaida lakini kwa kawaida huwa anaweza kutokwa damu kiasi kidogo sana, (inaweza kuwa kitone tu).

“Huweza kugundulika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, lakini changamoto ni kwamba wengi huwa hawachukui hatua kwenda kuchunguza hali zao,” anabainisha.

Anasema sera na miongozo huundwa kwa kuzingatia masuala ya tamaduni, imani, mila na desturi katika nchi husika.

UHUSIANO WA MTOTO

Anasema kwa kawaida wazazi wanao uwezo wa kutengeneza uhusiano (bond) na mtoto au watoto wao, waliopandikizwa katika tumbo la mama mwingine baada ya kuzaliwa.

“Kwa sababu, kibaiolojia mtoto au watoto genetically anakuwa wa wale waliotoa mbegu na yai, yule mama mwingine anakuwa ametumika tu kama ‘kibebeo’, bond inaweza kutengenezwa baada ya kuzaliwa,” anasema.

Anaongeza “Jinsi ilivyo, mtoto anapokuwa tumboni mwa mama ni kama vile hayupo tumboni mwake, Mwenyezi Mungu aliumba akijua kwamba mtoto yule hana msaada.

“Hivyo, alitengeneza mazingira ambayo atakuwa salama akiwa tumboni mwa mama, ndiyo akatumia njia ya kuweka ujauzito,” anasema.

Daktari huyo anasema lile kondo la nyuma ndilo ambalo hufanya kusiwe muunganiko wowote kati ya mama na mtoto.

“Yaani, kupitia kondo la nyuma, hakuna kitu chochote kinachoruhusiwa kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto isipokuwa kuruhusu kupitisha chakula na hewa tu.

“Hakuna muingiliano wa damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kondo linafanya kuwe na kitu kama ukuta, damu kutoka kwa mama ikifika pale haipiti itarudi kwa mama, kadhalika ya mtoto haitapita.

“Pale huruhusiwa kupita chakula na hewa ya oksijeni pekee ambayo mtoto hupokea ili aishi kipindi chote anakupokuwa tumboni mwa mama,” anabainisha.

Anaongeza “Hii ndiyo maana unakuta, kwa mfano, mama anaweza kuwa na maambukizi ya HIV lakini mtoto anazaliwa akiwa hana maambukizi.

“Aidha, mara nyingi mtoto huchukua group la damu la baba yake, lakini hata likiwa tofauti na lile la mama yake mtoto huishi.

“Lakini kwa mfano kama mama group lake ni B ikatokea ameongezewa damu ya group A anaweza kupoteza maisha, au wakati mwingine unakuta mtoto amekufa tumboni lakini mama asiweze kujua zikapita hata wiki mbili, ni kwa sababu hakuna muingiliano, ” anafafanua.

BENKI ZA UZAZI

Anaongeza “Kwa hiyo, yule mama mwengine anakuwa ni ‘kibebeo’ tu, vinasaba anavyorithi mtoto vinakuwa vya wale wazazi wa asili ambao wamechukuliwa yai na mbegu.

“Wazazi wanakuwa wanaingia mkataba na kumlipa mama mwengine anayebeba mimba,” anasema.

Anasema zipo pia nchi nyingine ambazo zimetengeneza sheria zinazosimamia kuruhusu watu kuweza kuuza mbegu zao za uzazi.

“Hasa nchi zilizoendelea, watu wanauza mbegu za uzazi, sheria zinasimamia hilo, maana unakuta kwa mfano mwanamke amekuwa mtu mzima, hajazaa, anahitaji kupata mtoto na hana mtu wa kumuoa.

“Lakini kuna wanaume wanauza mbegu kupitia ‘spam bank’, zinavunwa, zinahifadhiwa na zinakuwa zimeainishwa sifa za mbegu husika.

“Wanaandika tabia za mtu ambaye alichukuliwa mbegu hizo, kimsingi tabia na uwezo wa akili, mtoto hurithi kutoka kwa wazazi wake.

“Akili na uwezo wa mtu upo ‘related’ na uwezo wa ‘genes’ kutoka kwa wazazi, ndiyo maana zamani wazazi walikuwa wanazuia watoto wao kuolewa katika familia fulani fulani, kwa sababu vinasaba hurithiwa,” anasema.

Anaongeza “Hivyo, mtu hununua mbegu kulingana na sifa zilizoainishwa.

“Wenzetu wapo mbali, wanatunza mpaka mayai, kwa mfano mwanamke unakuta anaugua saratani ya kizazi anahitaji kufanyiwa tiba ya mionzi, na ile inaweza kumletea athari.

“Wanavuna mayai mengi wanayahifadhi, yanaweza kukaa hata miaka 100, baada ya matibabu, akipona, akitaka kuolewa wanachukua yale mayai yake na mbegu za mwanaume, wanapandikiza, mtoto anapatikana hana tatizo lolote,” anasema.

************MWISHO**********

Wanawake watahadharishwa kujisafisha kwa ‘toilet paper, tishu’

NA VERONICA MREMA – DAR ES SALAAM

KUJISAFISHA kwa kutumia ‘toilet paper au tishu’ baada ya kutoka haja inaweza kuchangia mwanamke kuishia kupata matatizo ya uzazi ambayo yanaweza kusababisha ashindwe  kushika mimba, siku zijazo kwenye maisha yake.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Vincent Tarimo alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na JAMVI LA HABARI katika mahojiano maalum.

Mahojiano hayo yamefanyika ikiwa ni siku kadhaa tangu, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alipotangaza kwamba hospitali hiyo inatarajia kuanzisha huduma ya upandikizaji mimba.

 

 

DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Vincent Tarimo amesema ….

 

 

Wengi wanapata infection kwa kufanya ngono na wanaume wengi, mwanamke anaposhiriki tendon has a vijana wadogo, bahati mbaya uke upon katibu na njia ya haja kubwa, uume hauna macho, mwingine anaenda anajifuta na tishu paper... Unaona umetakakata.  Nusa ile nguo yako utaoba ina harufu, 

 

 

 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement