
Mpigapicha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.
Taarifa zinasema marehemu alikuwa ametoka kazini jana usiku, akagongwa na gari maeneo ya Mwenge na kuvunjika miguu yote miwili na mkono mmoja.

Blog ya matukionamaisha inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki,
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Amen.
Chapisha Maoni