moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Wetu

Shule ya Msingi Msufini iliyopo Kijiji Cha Miono Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imepokea msaada wa mashine moja ya kudurufu na nyingine ya kuchapisha makaratasi zenye thamani ya Sh Milioni 2,600,000.

Mashine hizo zimetolewa na mdau wa maendeleo wa Amara Executive Lodge ikiwa ni sehemu ya kurudisha hisani kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Hotel hiyo, Karim Rutwengwe amesema kuwa, wakati wa mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika Oktoba 9 Mwaka huu.

Miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa ni pamoja na ukosefu wa mashine hizo shuleni hapo, jambo ambalo limewafanya kutatua changamoto hiyo.

"Leo tumekabidhi mashine mbili, Moja ya kudurufu makaratasi na nyingine ya kuchapisha ambazo zote zina thamani ya Sh Milioni 2,600,000.

"Msaada huu ni sehemu ya kurudisha hisani kwa jamii katika nyanja mbalimbali za afya, elimu na maendeleo ya jamii, Kwa sababu ni jukumu letu kufanya hivyo,"amesema Rutwengwe.

Ameongeza kuwa, mkakati wao ni kuendelea kushirikiana na jamii nzima ya Wana Chalinze ili kutatua changamoto zilizopo pamoja na kushikana mkono pale inapohotajika.

" Mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa, watoto wanaosoma katika Halmashauri ya Chalinze wanapata mahitaji muhimu ikiwa ni sehemu ya kuwafanya wasome vizuri, hivyo basi tutaendelea kutoa misaada mbalimbali ya kiutu na kijamii ili kukuza sekta ya elimu, "amesema.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bless Kanuti amemshukuru mdau huyo na kusema kuwa, awali walikuwa anapata tabu ya kudurufu makaratasi pindi wanapotaka kufanya mitihani, lakini mashine hizo zitaweza kuwasaidia kukabiliana na hali hiyo.

" Awali, tulikua tunapata tabu ya kuchapisha mitihani pamoja na kudurufu, msaada wa msaada huu ni mkubwa Kwa sababu umetusaidia kupata vitendea kazi tukiwa shuleni,"amesema Mwalimu Kanuti.

Ameongeza kuwa, mkakati wao ni kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wanafunzi ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani Yao, jambo ambalo kitawasaidia kuongeza ufaulu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement