moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Wetu - Chalinze

Shule ya Sekondari Chalinze iliyopo Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imepokea msaada wa kompyuta mpakato tano ambazo zimetolewa na mdau wa maendeleo kupitia Royal Splash Hotel na Splasha lounge zilizopo kwenye Halmashauri hiyo.

Akikabidhi msaada huo. Meneja wa Royal Splash Hotel na Splash Lounge bwana  Cosmas Michael amesema kuwa, kompyuta hizo ni sehemu ya mchango unaotokana na uwekezaji wa hotel hiyo katika eneo la chalinze ili kuhakikisha wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wanatumia zana za kisasa za kujifunzia ikiwamo kompyuta.

" Kama mdau wa maendeleo, tumefurahi kutoa msaada huu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaosoma kupitia zana za kisasa ikiwamo kompyuta mpakato, tunajua uhitaji ni mkubwa, lakini tumeanza na hiki kidogo ambao kwa Sasa kitawasaidia wanafunzi kusoma huku tukiendelea kutoa misaada mingine pale inapohotajika.

" Mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa, vijana wanaomaliza katika Halmashauri ya Chalinze wanapata elimu Bora Kwa ajili ya kuwasaidia kujiunga na vyuo vikuu, jambo ambalo kitawasaidia kuingia kwenye soko la ushindani la ajira ndani na nje ya nchi," alisema Michael.

Aliongeza kuwa, hotel ya Royal Splash na Royal lounge ni sehemu ya uwekezaji unaofanyika katika Halmashauri ya Chalinze ili kutoa huduma bora za malazi,Chakula, vinywaji, burudani, kuogelea na michezo mbalimbali ya watoto, hivyo basi waliwataka wananchi kuwaunga mkono.

Aliongeza kuwa,  uwekezaji huo umesaidia kutoa jira kwa vijana 25  kutoka ndani na nje ya chalinze na kupunguza tatizo la upatikanaji wa ajira kwa baadhi ya vijana.

"Tutaendelea kutoa msaada na kutoa ajira kulingana na uhitaji uliopo, hivyo basi tunaomba wananchi mtuunge mkono katika shughuli zetu za kibiashara ili tuweze kuinuana kimaendeleo,"aliongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Chalinze, Mwalimu Melkisedeki Komba aliishukuru hotel hiyo na kusema  kuwa, wamekuwa mstari wa mbele kuchangia kwenye shughuli za  maendeleo.

" Kwanza nitoe shukrani zangu kwa niaba ya bodi ya wadhamini, walimu na wanafunzi wote wanaosoma shule ya sekondari Chalinze kutokana na msaada huu mkubwa wa kimaendeleo ambao utawasaidia wanafunzi kusoma Kwa vitendo.

" Sasa hivi elimu ipo kiganjani, shule nyingi zinatumia kompyuta kwa ajili ya kuwafundishia watoto wetu, hivyo basi msaada huu utasaidia kupunguza pengo la uhaba wa vitendea kazi ikiwamo kompyuta na wanafunzi wanatapa elimu bora itakayowasaidia katika soko la ajira,"alisema Mwalimu Komba.

Kwa upande wao Wanafunzi wa Shule hiyo wameushukuru Uongozi wa Royal Splash Hotel na Splash lounge kwa msaada huo utakaowasaidia kusoma kwa vitendo.

Royal Splasha Hotel na Splasha lounge zinahakikisha kuwa  asilimia 10 ya mapato, yanachangia kwenye miradi ya maendeleo na jamii ya Chalinze. Wanapatikana Kwa namba 0790 129 503

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement