Uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za tiba [dawa, chanjo, vifaa tiba na vitendanishi] ndani ya Tanzania umeendelea kupigiwa 'chapuo' na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania [TMDA].
Tanzania inashiriki Kongamano na Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Dawa, Vifaa Tiba, Chanjo na Vitendanishi (CPHI) yanayofanyika Milan, Italia, tarehe 6–8 Oktoba 2026.
Maafisa wa TMDA wapo katika mkutano huo na sasa ushiriki umefungua fursa muhimu kwa Tanzania kukutana na wawekezaji na wadau wakubwa wa sekta ya bidhaa tiba duniani.
Chini ya mwavuli wa Kikosi Kazi cha Kuharakisha uanzishaji wa viwanda tiba nchini (PIAT), ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara wa Afya, Emmanuel Tayari.
Hatua hii inaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi wa bidhaa tiba kutoka nje, sambamba na kuimarisha upatikanaji wa bidhaa tiba bora na salama kwa afya ya jamii.




Chapisha Maoni