moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum

Barua ya mwaliko imetumwa M24 TANZANIA Media, kushiriki Mkutano wa 5 wa kimataifa wa ngazi ya juu wa Mawaziri kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa [Antimicrobial Resistance - AMR].

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Abuja Nigeria Desemba 6 hadi 8, 2026. Mwaliko huo umetolewa kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Nigeria kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Lengo kuu ni kuimarisha hatua za kimataifa za kukabiliana na tishio la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Veronica Mrema kupitia jukwaa la M24 TANZANIA ambapo amekuwa akichapisha habari na makala ambazo zinaangazia AMR anatarajiwa kuwa miongoni mwa waandishi wa habari watakaohudhuria.

Mkutano huo unafanyika wakati AMR ikiendelea kuwa changamoto ya kimataifa inayohitaji ushirikiano wa sekta mbalimbali. 

Mkutano wa Abuja utatumia mtazamo wa One Health unaounganisha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira katika kukabiliana na tishio hilo. Mkutano huo utafanyika Disemba 6 hadi 8, mwaka huu.

M24 TANZANIA imekuwa ikifuatilia na kuripoti masuala yanayohusiana na AMR, ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya dawa, matumizi holela ya dawa zenye asili ya kulevya na changamoto ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Habari na Makala alizoandika kuhusu AMR zinapatikana kwa undani na kina zaidi kupitia link hii  Makala za M24 Tanzania kuhusu AMR. 

M24 TANZANIA pia imeendelea kuangazia umuhimu wa matumizi sahihi ya dawa na nafasi ya udhibiti wa dawa katika kupunguza hatari zinazoweza kuchangia usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu wa afya, watafiti, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, vyombo vya habari na wadau wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kujadili hatua za kuharakisha utekelezaji wa ahadi za kimataifa za kukabiliana na AMR.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement