moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Ustawi wa watu [wellness] mahala pa kazi ni suala linalopaswa kupewa kipaumbele ili kuwa na kizazi bora na kufikia malengo mahususi kwa jamii na Taifa kadhalika pamoja na maendeleo endelevu ya dunia nzima.

Mtu ambaye hana ustawi mzuri wa afya ya akili na mwili nao hukosa ushirikiano ipasavyo mwisho wake ni kuishia katika magonjwa mbalimbali hasa yasiyoambukiza [NCDs].

Hali hiyo huathiri utendaji kazi mzima wa mtu husika muda mwingi huishia katika kutibu magonjwa, kukosa utulivu wa nafsi na hata ma-kampuni kupata hasara badala ya faida waliyoitarajia.

Taasisi ya Bloom Wellness Tanzania imeliona pengo kubwa katika suala la ujenzi wa ustawi bora wa afya ndani ya jamii, watu waliopo ofisi mbalimbali na sasa imeamua kuchukua hatua ya ziada.

“Tumeamua kuanzisha wiki ya ustawi Tanzania [Tanzania Wellness Week] itakayofanyika Julai 1 & 2, 2025,” amesema Sophia Byanaku Mkurugenzi Mkuu wa Bloom Wellness Tanzania.

Ni wakati wa uzinduzi kuelekea wiki hiyo ya ustawi, tukio ambalo limefanyika mapema leo Mjini Dar es Salaam ukumbi wa kimataifa wa JINCC.

Byanaku amesema katika wiki hiyo ya ustawi wamekusudia kuwaleta pamoja wadau wengi zaidi ili kuwa na mjadala mpana zaidi kuangazia kwa kina suala la ustawi agenda Kitaifa.

“Wizara ya Afya ndiye mdau mkuu anayeangalia ustawi wa afya nchini tanzania, tumepata ushirikiano mkubwa na wamekubali kuwa ‘supporter’s’  wetu ili kuweza kufanya hili jambo kwa pamoja,”.

Amesema na kuongeza “Lengo [la wiki ya usttawi Tanzania] ni kuwaita hawa wadau kwa pamoja ili kwenda kuzungumza kwa pamoja na kuweka sauti moja ili kuleta mwamko na mabadiliko ya pamoja.

“Wizara ya afya ni mdau namba moja, kuna watafiti kwa sababu tunaamini suala hili la ustawi hatuna data za kutosha.

“Ndiyo maana inakuwa ngumu sana kwa makampuni kuweza kuwekeza kwenye suala hili [si kama ilivyo kwa magonjwa mengine] kama Ukimwi, TB na Malaria.

“Ni vitu ambavyo vina takwimu za kutosha na ndiyo maana imekuwa makampuni na jamii kufanya hizi program kwenye sehemu zao lakini ukienda kwenue suala la ‘wellness’ kuna changamoto.

“Kwa sababu mwajiri haoni umuhimu wa kuwekeza pesa katika hili suala kwa sababu hamna data, hamna ukweli inakuwa ngumu sana,” amesema.

Byanaku amesema watu wengine [wanaoshiriki wiki hiyo ya ustawi Tanzania] ni wadau kutoka kada mbalimbali zinazohusika ikiwamo wa lishe, afya ya akili na sekta zisizo za kiserikali.

“Tunataka tuwaweke pamoja tuongee kwa lugha moja tuelewane tuwe wa-moja [kuna] na watu wa Sera pia.

“[Kwa sababu] kama hakuna data hakuna Sera na kama hakuna Sera hakuwezi kuwa na bajeti ya hili suala.

Ameongeza “Ndiyo maana tunataka tuwalete wadau kwa pamoja tuongee, tuone changamoto zipo wapi kwa hili suala na sauti ikitoka kwa pamoja italeta nguvu na tija na itakuwa mabadiliko kwa wote.

Byanaku amedokeza zaidi, “[‘Wellness’] ni gurudumu ambalo lina vipengele vingi sana, afya ya akili ni kipengele kipo kwenye gurudumu kubwa linalohusu afya.

“Kama masuala ya fedha hayapo vizuri, lishe haipo vizuri, magonjwa ya moyo, kisukari  na mengine yasiyoambkiza ukiugua sana utaangukia kwenye magonjwa ya akili pia.

“Lakini pia changamoto ambazo tunazipata sehemu za kazi [wasiwasi, msongo wa mawazo] hivi vyote visipoangaliwa unaweza kipata changamoto/tatizo au magonjwa ya akili,” amesema.

Amesema hali kwa Tanzania changamoto ipo, takwimu zipo lakini hazipo kwenye mpangilio.

“Unakuta ni taasisi moja moja tu inafanya hizi ‘study’, kuna zingine [matokeo yake] hayajatoka nje kwa jamii / hadhira.

“Ili watu waweze kuelewa hii changamoto, tunachukulia 'wellness' kama anasa hivyo watu hawaoni ulazima wa kuwekeza katika hilo.

“Tumeona hilo na kuamua kuwa wabunifu kuanzisha ili, tafiti nyingi tunatumia data ambazo ni za nje, inatuwia vigumu kwa taasisi au jamii kutruelewa kwamba hii changamoto ipo kwa ukubwa gani.

Ameongeza “Ni kitu nimekuwa nikiongea [kuelimisha jamii kwa namna mbalimbali, lakini] sasa tumeamua kuongea kwa vitendo na kujumuisha watu wote.

“Watufungilie milango na walete watumishi wengi kwenye tukio la julai na tutakuwa na matukio mengi kuelekea kwenye kilele.

“Tukitaka ‘support’ yao watukaribishe ili siku ya kilele tuweze kupata uelewa wa pamoja, mwamko wa waajiri upo lakini wanataka kufanya lakini si kwenye kupata matokeo,” amesema.

Ameongeza [Waajiri wengi] wanafanya [program za wellness] ila hawafanyi vile inavyotakiwa ili kuleta matokeo chanya.

“[Lakini] sitaki kuwalaumu … kama nilivyosema kwanza hatuna takwimu, hatuna data,” amesema na kusisitiza zaidi,

“.., ndiyo maana tunaleta tukio la pamoja ili wakiwekeza wajue wanawekeza kwenye kitu ambacho kitakuwa na faida kwetu [wazungu wanasema ‘return of ivenstiment’,”.

Byanaku amesema nchi zilizoendelea nyingi zimepata mafanikio makubwa kwa kuwekeza katika ustawi wa watu.

Akitolea mfano taifa la Marekani amedokeza “Ipo juu kwenye suala la program za ustawi wa afya sehemu za kazi.

“Ma-kampuni mengi ambayo yapo mbele kwenye kufanya vizuri, kutengeneza ‘profit’ nzuri wamewekeza kwenye ‘wellness’ hata google wana kitengo kabisa [cha wellness].

“‘Return of investment’ [ya google]  ni kubwa kwenye kutengeneza pesa na kufanya vizuri kidunia wapo vizuri,” amesisitiza.

Mtaalamu wa Mabadiliko ya Tabia na Mawasiliano ya Afya kutoka Idara ya Kinga, Wizara ya Afya ameipongeza hatua ya Bloom Wellness Limited kuanzisha jambo hilo.

“Si kitu kigeni, lakini kizuri kwa jamii yetu ya sasa ya Tanzania, mtakuwa mashahidi changamoto ya Magonjwa Yasiyoambukiza [NCDs] ni kubwa nchini mwetu hivi sasa.

“Magonjwa ya akili, kisukari, shinikizo la damu, ajali na saratani imekuwa changamoto kubwa kwa binadamu, familia na taifa kwa ujumla,” amesema.

Ameongeza “.., wameona ni kitu wasikae nacho wenyewe wakitoe kwa wengine ili waweze kujifunza.

“Tunasema afya yako mtaji wako, inatakiwa kusikiliza wataalmu pia kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kuweza kufikia hilo lengo la kusema afya yangu mtaji wangu,”.

Grace amesema Waziri Mkuu wa Tanzania alizindua mwongozo wa ufanyaji mazoezi mahala pa kazi jambo ambalo Wizara hiyo inalisimamia ipasavyo.

“Sisi Wizara ya Afya tunatekeleza tunayo program inasimamia mazoezi mahali pa kazi, Ofisi ya Rais TAMISEMI pia ina hizi program.

“Tuna Taasisi ya Afya ya Akili - Mirembe imekuwa ikitoa elimu kwa njia ya mtandao, ‘social media’ na kuna wakati inaitisha watumishi wa Serikali kuwapa elimu bure kabisa,” amesema.

Amesisitiza “Serikali inahakikisha wafanyakazi wake wanapunguza uwezekano wa kupata magonjwa NCDs.

“Lakini kuanzisha na kuhamasisha ni jambo moja lakini je mtu binafsi anafanya / anatekeleza hiyo ni changamoto, sisi wenyewe tuone umuhimu wa kuyazingatia ili tujenge afya zetu,” amesema.

Tukio hilo la uzinduzi limetanguliwa na mdahalo wa wazi uliowaleta pamoja wataalamu mbalimbali wa afya, lishe, fedha, waandishi wa habari pamoja na wakuu wa taasisi za Umma na binafsi.

1 Maoni

  1. Kazi Yako ni njema katika kuelimisha Jamii kiukweli me najifunza mengi kupitia ukurasa huu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement