Kwa mara ya 22 sasa Mwanahabari wa Clouds Media Group (CMG) Dixon Busagaga anaweka rekodi nyingine ya kupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi Barani Afrika.Busagaga ni mwakilishi wa CMG Kanda ya kaskazini ameendelea kuweka rekodi yake ya kipekee tangu alipoanza safari zake mnamo mwaka 2012.Alikuwa miongoni mwa kundi la watu 300 wakiwemo waandishi wa habari waliopanda Mlima huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.Wakati huo huo Clouds Media Group (CMG) ikiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.
Chapisha Maoni