moja

Responsive Advertisement



Na Mwandishi Maalum

Umahiri katika uandishi wa habari za Magonjwa Yasiyoambukiza [NCDs] Tanzania, mchango wa Veronica Mrema umetambuliwa na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania [TANCDA].

Ni katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa TANCDA ambayo yalifanyika huko Coco Beach Nov. 30, 2024.

Yalienda sambamba na matembezi ya kuchangamsha mwili [jogging] yaliyofanyika kuanzia Coco Beach kupitia daraja la Tanzanite hadi njia panda ya Agakhan kisha kurejea tena Coco Beach.

Cheti hicho amekabidhiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Afya ya Akili na Ajali wa Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu ambaye alihudhuria maadhimisho hayo.

"Tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na waandishi wa habari katika kuandika masuala haya ya Magonjwa Yasiyoambukiza nchini," amesema Dkt. Ubuguyu.

Veronica ni miongoni mwa waandishi wa habari wanaoshiriki moja kwa moja katika uelimishaji jamii kuhusu NCDs.

Magonjwa hayo ni pamoja na ya moyo, figo, saratani, kisukari, shinikizo la damu, Siko Seli, kiharusi, magonjwa ya akili na yake yatokanayo na ajali mbalimbali hususan za barabarani na mengineyo yaliyo kwenye kundi hilo.

Pia amekuwa akifanya uchechemuzi katika mada za NCDs akichochea kuleta mabadiliko ya tabia kwa jamii na maboresho ya Sera za afya Tanzania, kwa miaka mingi sasa. 

Pamoja na cheti hicho, ndiye Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo ya EAMNA ambayo ilitambua waandishi wa habari mahiri Afrika Mashariki wanaoangazia magonjwa hayo ndani ya jamii zao.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza na EANCDA ambalo ni Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Afrika Mashariki 

"Namshukuru MUNGU kwa kupata cheti hiki maalum na ninawaahidi kuendelea kuwapa habari na makala bora zaidi wasomaji wa M24 TANZANIA MEDIA," amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement