moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum

Barani Afrika tasnia ya habari zinazojikita katika ulimwengu wa sayansi na afya inakua kwa kasi huku ikihitaji uandishi wa weledi, ubunifu na ushahidi wa ki-sayansi kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.

Kwa muktadha huu, unafanyika Mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari za Sayansi [World Conference of Science Journalists - WCSJ2025].

M24 TANZANIA MEDIA ni katika ya wale ambao wamechaguliwa kushiriki mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Desemba 1 - 5, 2025 huko Pretoria Afrika Kusini.

Ushiriki huu umewezekana baada ya mwanzilishi wa M24 TANZANIA MEDIA, Veronica Mrema, kuchaguliwa kupata udhamini wa safari [Travel Grant] kutoka Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ya Afrika Kusini [DSTI].

Katika barua rasmi iliyotumwa, DSTI imeeleza "Tunakupongeza kwa dhati kwa kuchaguliwa kupata udhamini wa safari wa DSTI kuhudhuria Mkutano wa Waandishi wa Habari za Sayansi [WCSJ2025] kutokana na idadi kubwa ya maombi, tunajivunia kukuunga mkono kushiriki kwako katika tukio hili la kimataifa lenye heshima".

DSTI pia imempatia udhamini huo Veronica kwa kuvutiwa na utendaji kazi wake katika upashanaji habari za ki-sayansi na afya, ikimtambua pia kwa nafasi ya uongozi akiwa Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam [DAR-PC) na Afisa Habari wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Siko Seli Tanzania [SCDPCT].

Akizungumza Veronica amesema "Kupitia mkutano huu, nia yake ni kupeleka sauti ya Tanzania kimataifa, kuandika habari za kina zinazolenga afya, sayansi na teknolojia na kujifunza mbinu mpya zitakazoboresha maudhui ya M24 TANZANIA MEDIA kwa manufaa ya jamii".

Mkutano wa WCSJ2025 utakutanisha mamia ya waandishi, wanasayansi, watafiti, wahariri na taasisi za mawasiliano kutoka nchi zaidi ya 80 ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa huku pia kukiwa na mdahalo maalum kwa ajili ya waandishi wa Ukanda wa SADC. 

Ushiriki wa M24 TANZANIA MEDIA unalenga kuimarisha ubora wa taarifa zake za afya na sayansi sambamba na kujenga mitandao ya ushirikiano na vyombo vya habari na taasisi za kimataifa.

Ushiriki huu unafungua ukurasa mpya kwa Tanzania katika kuonesha uwezo wa vyombo vya habari kusimulia masimulizi ya kisayansi kwa lugha nyepesi, sahihi na yenye kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement